Jinsi ya

Jinsi za Kujifunza Computer

Katika hatua hii ya kwanza utajifunza kuhusu kampuni ya Microsoft na historia fupi ya waanzilishi wake. Utajifunza sehemu kuu za kompyuta ambazo ni KIU (Kitengo kikuu cha uchakataji) au CPU (Central Processing Unit), Monita, puku, bodidota na printa. Mfululizo wa masomo haya utakujengea msingi wa kuanza kutumia kompyuta hasa matumizi ya programu za Microsoft ofisi kama vile Microsoft Word, Microsoft powerpoint, Microsoft publisher, Microsoft Excel n.k.

Kampuni ya Microsoft ni kampuni ambayo hutengeneza programu za kompyuta kwa ajili ya watumiaji wa kompyuta duniani kote. Ilianzishwa mnamo mwaka 1975 na Bill Gates kwa kushirikiana na Paul Allen. Programu ambazo hutengenezwa na kampuni hii ni pamoja na windows, Microsoft office (kama vile, Microsoft word, Powerpoint, Publisher n.k), internet exproler (Programu ya kuingilia katika mtandao wa intaneti), websaiti ya Microsoft ijulikanayo kama Microsoft Network (MSN) ambayo hutumika kuingilia kwenye mtandao wa intaneti n.k. Baadhi ya programu za Microsoft kama vile mfumo wa Window wa uchakatuaji (Windows operating system) huwa zimekwisha ingizwa mara mtu ananunuapo kompyuta. Mtu aweza kununua na kuingiza nyingine kulingana na uhitaji wake.

Leave a Reply