Teknolojia

Je wajua Jinsi ya Kuondoa Lock Pattern ama Password Uliyoisahau katika Android

zipo njia nyingi kutegemea na aina ya simu au toleo la Android ambalo simu yako inatumia.

Simu zote ambazo zinatumia Android Kitkat ambayo ni toleo la 4.4 na nyingine zote ambazo ni matoleo ya nyuma ya hili zenyewe ni rahisi pindi unaposahau password yako, katika kundi hili la simu pindi tu unaposahau pattern ama password yako simu yako itakutaka uingize barua pepe na password yako ya Google ambayo ulijiandikishia katika simu hiyo na kisha simu yako itafunguliwa.

Angalizo! njia hiyo itafanya kazi iwapo umewasha data katika simu.

 

Kwa kutumia Android Device Manager

Njia hii simu zote ambazo katika zimewezeshwa programu hii, vile vile njia hii itafanikiwa iwapo tu wakati huo intaneti ya simu itakuwa imewashwa. njia hii inaweza sio tu kubadilisha password ya simu kwenda katika password yako mpya ila pia inaweza kusaidia kufuta mafaili yote yaliyo ndani ya simu – hii ni muhimu kama simu imepotea au kuibiwa.

Fuata hatua zifuatazo kufungua simu uliyoifunga.

 1. Tembelea google.com/android/devicemanager kupitia katika simu nyingine ama kompyuta
 2. Ingia kwa kutumia barua pepe pamoja na password yako uliyotumia kusajilia katika simu iliyojifunga
 3. Tafuta na chagua kifaa ambacho unataka kukifungua (maana kama una vifaa zaidi ya kimoja  ulivyo visajili katika huduma hii vyote vitaonekana hapa)
 4. Chagua Lock na uinigize password ya muda kisha bonyeza Lock tena
 5. Baada ya hapo unatakiwa uone meseji ikithibitisha kuwa kufaa chako kimebadilishwa password
 6. Wakati huu katika simu utaona sehemu ya kuandika password inatokea hapa jaza ile password yako mpya.
 7. Ingiza pasword na uende moja kwa moja kuiondoa pasword hiyo ya simu yako.

2 Comments

  1. kama unatumia compyuta ndio itakua vzur zaid,,,,

   unapress( CTRl + P) kwa wakat mmja hii ni shortcut kwa ajir ya kuprint document au unaweza right click kwenye mouse then uchague print……

   nahic hii ni option nzuri kama hakuna option ya kudownload

Leave a Reply