Jinsi ya

Ficha Folders na Files Zako – Bila Kutumia Program

Kwa kawaida kila mtu anahitaji usiri katika mambo yake anayofanya, si kila kitu lazima kifaamike kwa watu au marafiki zako ambao kwa namna moja ama nyingine wanaingia katika komputa yako.Password (Neno la siri) tu katika akaunti yako kwenye komputa haimaanishi kwamba vitu vipo salama. Bado mtu anaweza akawa na password na akafuta,akabadili,au akaiba mara tu apatapo neno lako la siri).Kwa hyo kuna vitu ambavyo wapaswa kuvijua lakini wengine wasijue hali ya kuwa mtatumia pamoja komputa.Hivyo ni vyema kuviweka katika sehemu na kuficha.

Hivyo nitakuelekeza njia rahisi ambayo haiitaji kutumia program yoyote bali tu ni sifa mojawapo ambayo ipo katika mfumo wa komputa (operating system)/windows.Baadhi yenu mtakuwa mnafaamu na wengi zaidi hawafaamu,na huenda wanahangaika na kutumia program. hvyo nita share kama ifuatavyo.

HATUA ZA KUFICHA FOLDERS.

 1. Nenda katika sehemu ambayo lipo folder lako ambalo ungependa kulihifadhi lisionekane, na kama yapo mengi basi chagua yote (select all of them).-kumbuka sehem (location) ulipohifadhi hilo folder, muhimu.
 2. Right click kwenye folder/folders ambazo umechagua kuzificha,chagua option properties (ipo mwisho kabisa) halafu itafunguka window ndogo yenye maelezo/details lakin chini kabsa kuna sehem imeandikwa “Attributes”, hapo utaona kiboksi kidogo (checkbox) kwa mbele kuna neno “Hidden”, kwa hyo hicho kiboksi utaclik mara moja (check it).
 3. Baada ya hapo, utabonyeza kitufe OK, na utahakiki mabadiliko kwa kuchagua penye “Apply changes to this folder ,subfolders and files” na utamalizia tena kwa ku click OK.
 4. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuficha folder zako ambazo ulizichagua hapo awali na katika hiyo sehem hazitaonekana tena kwa hyo kwa mtu ambaye ni mtumiaj wa komputa yako wa kawaida hawezi kujua kama vipo pale hivyo vitu.

HATUA ZA KUZIONA FOLDERS ULIZOFICHA.

 1. Utafungua windows explorer na kwenda kwenye menu ambazo zipo juu kwenye toolbar setting “(Organise->folder options and search options)”,itafunguka window ndogo yenye tabs tatu “(General, View and Search)”.
 2. Baada ya hapo cha kufanya shuka chini na uchague sehemu imeandikwa “Show hidden files, folders and drives” na ukclik ok.
 3. Utakuwa umemaliza na sasa waweza kwenda sehemu husika ambapo lipo folder/folders utazikuta zipo pale. Tofauti yake na zingine zenyewe zinaonekana kama zimefifia kwa mbali.waweza kufanya chochote unachohitaji kufanya.
 4. Na baada ya hapo utarudi kwenye hatua 1 na ya 2 na utachagua kwenye “Dont show hidden files, folder and drives” ili uendelee kuzificha.

HATUA ZA KUFICHUA FOLDER ZIONEKANE.

Utakapohitaji kubadil mawazo sasa hauhitaji tena kuficha folders,yaani ziwe kama ilivokuwa mwanzo utaanza kama ifuatavyo

 1. Fuata hatua za kwenye “HATUA ZA KUZIONA FOLDERS ULIZOFICHA” mpaka hatua ya 2.
 2. Nenda kwenye sehemu ambapo umehifadhi chagua ambazo zilikuwa zimefichwa
 3. Right click, chagua “properties”. kitakuja windows ndogo hvyo utaenda mpaka kwenye “Attributes” na utatoa tick ambayo ipo kwenye “Hidden” click ok. utakuwa umefanikiwa kurudi katika hali ya mwanzo.

FAIDA ZA NJIA HII

 1. Ni njia rahisi ambayo haiitaji kutafuta program na kuanza kuiweka kwenye komputa, kwani kuweka program nyingi kwenye komputa ni kuibebesha mzigo na kuifanya kuwa nzito
 2. Hauhitaji kuwa na kumbukumbu ya password ili kuweza kuona ulichoficha.
 3. Inapunguza matumizi ya nafasi iliyopo kwenye hard disk yako, unachokifanya ni setting tofauti na kuingiza program ambayo itahitaji nafasi
 4. Nzuri kutumia hasa unapohitaji kuficha baadhi ya vitu kwa watu ambao si wataalamu wa komputa.
 5. Ina saidia kutunza vitu, kutunza siri.
 6. Inafanya kazi hata kama ukiihamisha hard disk yako kwenye komputa yako ingne bado vitakuwa vimefichwa.

HASARA ZA NJIA HII

 1. Inahitaji uwe unakumbuka sehemu / location zilipo. sawa na kukumbuka passord kama ambavyo ungetumia program
 2. Alie mtaalamu wa komputa anaweza kuviona japo ni kwa shida kwa maana anakuwa hajui sehemu gan hasa vilipo. Hivyo atafanikiwa kufanya setting lakin itabidi atafute kila sehemu ili kuona.

Ahsanteni, Mshirikishe na mwezio..

 

One Comment

 1. Asante aise, very helpful. Nimeambiwa na mtu kuhusu hii website na nimetembelea nimekutana na ambayo katika maelezo yake baadhi imenisaidia. Issue ya hidden folders.

  Pia natamani kujua ukifuta vitu kwenye recycle bin unaweza ukavipata tena?

Leave a Reply