Habari Mpya, Ukristo

Faida Moja ya Mbeba Maono .

FAIDA YA MBEBA MAONO – Elimu kwa Wote.

Faida Moja ya Mbeba Maono.

Unajua hakuna aliyefanikiwa katika jambo lolote bila kuwa na nguvu ya kubeba maono ya nafsi yake. Kwa Tafsiri fupi maono ni kama alama ambayo mtu anaacha baada ya yeye kufikia hatua flani hata baada ya yeye mtu huyo kufariki. Najua unaweza ukawa na maswali Zaidi kuhusu maono ni nini, usisite kutuandika maoni yako na maswali kama unayo.

Kwanini Nakuandika hii Makala leo? Kwanini elimukwawote leo inakuandika faida ya mtu kuwa na maono?

Nia yangu nataka ewe msomaji hasa kijana au vijana kuwa kuna faida ya wewe kuwa na maono. Moja ya faida ya wewe kama kijana kuwa na maono ni “INAKUPA NIDHAM YA MAISHA”.

Nidhamu ya maisha kwa kijana mbeba maono ni kitu ambacho ni lazima awe nacho. Ninaposema Nidham Binafsi namaanisha kuwa na uwezo wa kuishi kulingana na hali ya maisha uliyonayo. Hauwezi ukawa una wazo la kufauru mithian harafu ushindwe kuwa na nidhamu ya kusoma kwa bidii, maana hata kama hutaki kusoma maono yanakulazimisha kusoma, hata kama umechoka yanakupa nguvu ya kuendelea kusoma.

Nakumbuka kipindi flani katika maisha yangu, nilipokuwa nasoma elimu ya High School, Old Moshi High School in Kilimanjaro. Nakumbuka nilivyokuwa nasoma hata leo nikifiri nabaki nashanga ni wapi nilipata nguvu ya kusoma kwa style ile niliyokuwa nasoma usiku na mchana. Unaweza ukawa shuhuda kwamba michepuo ya sayansi kama PCM na PCB inavyoongelewa na wanafunzi wengi hasa PCB. Binafsi nilikuwa nasoma PCM lakini nakumbuka ilifika kipindi hata kulala darasani wiki nzima.

Nataka Kusema Nidhamu ya Maisha niliyokuwa nayo katika kipindi kile ndiyo iliyonisaidia kufika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Kuchaguliwa Kusoma Shahada ya Elimu ya Uhandisi wa Kompyuta na Mifumo ya Mawasilano kwa miaka minne.

Mtumishi wa Mungu mmoja, Nchini Nigeria Bishop David Oyedepo aliwahi kusema “You can’t know were you’re going and not package or commit yourself to get their”

Wewe kama Kijana tazama maisha ya Mtumishi wa Mungu Yusufu, Alivyokuwa katika nyumba ya Potifa alijua hii ni njia ya mimi kufika katika kiti cha ufalme, iweje nifanye dhambi kubwa hii. Nguvu ya Nidham Binafsi aliyokuwa nayo ilikuwa imefichwa katika maono alikuwa amebeba. Hata alipokuwa gerezeni bado alikuwa na nidhamu binafsi hata ilimfanya baadae kuwa mkuu wa wafungwa gerezani.

Maono yanafaida ya kukupa Nidhami Binafsi

Tolei la 1.0